Dhima za Tungo za Malezi katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Tenzi Teule. (Swahili)

Item request has been placed! ×
Item request cannot be made. ×
loading   Processing Request
  • Additional Information
    • Abstract:
      Malezi ni suala muhimu katika jamii na ni dhamira iliyowashughulisha wanafasihi mbalimbali, ikiwamo utenzi. Makala hii imechunguza dhana ya malezi katika tenzi teule ambazo ni: Utenzi wa Mwanakupona, Howani Mwana Howani, Siraji na Utenzi wa Adili kwa kuzingatia malengo manne mahususi. Makala imechunguza dhima za tenzi teule kifasihi, kijamii na kwa watunzi wenyewe. Nadharia za Sosholojia ya Fasihi na Mwingilianomatini zimeongoza uandishi wa makala hii. Data za makala zimekusanywa kwa kusoma matini teule na machapisho mengine yanayohusiana na mada hii. Matokeo yanaonesha kwamba watunzi husika wamefanana na kutofautiana katika kuzungumzia malezi. Kwa watunzi wa kike, dhima zilizojitokeza ni kumcha Mwenyezi Mungu, kujipamba na tabia njema, maisha ya ndoa, utii kwa wazazi, usafi na umaridadi pamoja na umuhimu wa elimu na kazi. Kwa watunzi wa kiume dhima zilizojitokeza ni utiifu na heshima, mapenzi na ndoa, bidii katika kazi, elimu ya kujitegemea, uvumilivu, uadilifu katika ushahidi, kutunza siri na kutimiza ahadi. Kwa watunzi wote wa kike na kiume, dhima zilizojitokeza kwa kufanana ni mazingatio ya muktadha wa jamii, nafasi ya baba na mama katika malezi na ukamilifu katika malezi. [ABSTRACT FROM AUTHOR]
    • Abstract:
      Copyright of Kioo Cha Lugha is the property of University of Dar es Salaam, Institute of Kiswahili Studies (IKS) and its content may not be copied or emailed to multiple sites or posted to a listserv without the copyright holder's express written permission. However, users may print, download, or email articles for individual use. This abstract may be abridged. No warranty is given about the accuracy of the copy. Users should refer to the original published version of the material for the full abstract. (Copyright applies to all Abstracts.)